Rais wa Ukaine Volodymyr Zelensky ametembelea kwa mara ya kwanza eneo lililoharibiwa kwa vita kusini mwa nchi hiyo kujionea uharibifu uliofanyika pamoja na kuwashukuru wanajeshi wa nchi yake walio mstari wa mbele kwenye uwanja wa mapambano.

Katika ziara hiyo ya nadra kufanywa na kiongozi huyo nje ya mji mkuu Kyiv, Zelensky aliuzuru mji wa Mykolaiv ulio kwenye mwambao wa bahari nyeusi na kisha kuwatembelea wanajeshi karibu na eneo hilo na kwenye mkoa jirani wa Odessa.

Mji wa Mykolaiv ni miongoni mwa maeneo ya kimkakati yanayolengwa na Urusi kwa kuwa unapatikana kwenye njia ya kuelekea bandari muhimu ya Odessa kwenye bahari nyeusi.

Wiki za hivi karibuni vikosi vya Urusi vimewekeza nguvu kuyadhibiti maeneo ya kusini na mashariki mwa Ukraine ikiwemo eneo la bahari nyeusi.

NATO: Vita Ukraine na Urusi sio ya kuisha
Polisi yaonya matumizi mabaya mitandao ya kijamii