Shirika la Chakula Duniani (WHO), limesema Watu milioni 15 nchini Sudan wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, madai ambayo yanathibitishwa na ripoti ya pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Mkuu wa WFP nchini Sudan, Carl Paulsson imesema uhaba huo unatokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, mtikisiko wa kisiasa na kupanda kwa bei ya chakula duniani.

“WFP Sudan imekamilisha tathmini yake ya usalama wa chakula kwa bahati mbaya, hofu yetu zaidi imethibitishwa na tunakadiria kwa wakati huu kwamba watu milioni 15 wanakabiliwa na njaa nchini Sudan,” ilisema ripoti hiyo ya Paulsson.

Hata hivyo makadirio ya WHO ya mwaka 2022 yanaonyesha kuongezeka hadi kufikia takriban watu milioni 18, na kwamba tatizo hilo linatokana na vichochezi vikuu vya uhaba wa chakula, mzozo wa kiuchumi, migogoro, mavuno duni na athari za kimataifa.

Kulingana na madai ya Umoja wa Mataifa, viwango vya ufadhili vinapungua kukidhi mahitaji ya kibinadamu nchini humo, ambapo asilimia 40 ya wakazi wanatarajiwa kukumbana na uhaba wa chakula ifikapo Septemba 2022.

Naye mchuuzi wa soko, Badria Hussan Umar amesema sababu ya bei hizi kuwa juu ni migogoro na ni sawa na ilivyokuwa katika Tawila wa mwaka 2004 walipoua watu na kupora mali zao.

“Tulipofika hapa tulipokea msaada lakini sasa hivi umesimamishwa sasa mfano nikifanikiwa kuuza kitu basi naweza kula na nisipopata pesa za kutosha pia nalala njaa zaidi ya hayo hatuna chochote,” amesema Umar.

Mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba, 2021yalisimamisha mpito wa Sudan kwa utawala wa Kidemokrasia baada ya miongo mitatu ya ukandamizaji na kutengwa Kimataifa chini ya Rais wa kiimla Omar al-Bashir.

Zanzibar kuunda chombo cha usimamizi Serikali ya umoja wa Kitaifa
Serikali yatangaza mfumo mpya wa tozo