Ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Kassim Majaliwa nchini Cuba imeanza kuinufaisha Tanzania mara baada ya kukutana na Rais wa Shirika la Viwanda vya Sukari nchini humo, Francisco Lled, kwaajili ya kujadili namna ya uwekezaji wa kiwanda cha uzalishaji Sukari nchini.

Shirika la Sukari la nchini Cuba linauwezo wa linazalisha tani milioni nne za sukati kwa mwaka huku mahitaji ya ndani ni tani 700,000, ambapo kiasi kinachobaki huuzwa nje ya nchi, na kwa sasa shirika hilo linazalisha tani milioni mbili tu katika viwanda vyake 56.

Majaliwa amekutana na Lled wakati alipofanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha sukari cha UGB Central Azucarero 30 de Noviembre katika mji wa San Nicola’s de Bari ambacho ni kati ya viwanda 27 vya shirika hilo linalomilikiwa na Serikali ya Cuba kwa asilimia 100.

Amesema kuwa amemshawishi Lled kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kuzalisha sukari. ambapo amesema kuwa kwa sasa Tanzania ina viwanda vikubwa vitano vya sukari ambavyo uzalishaji wake hautoshelezi mahitaji ya ndani.

Kwa upande wake Lled amesema kuwa sera za Cuba haziruhusu shirika kwenda kuwekeza nje ya nchi na badala yake wanaruhusiwa kuzisaidia nchi zinazohitaji kujenga viwanda hivyo kwa kutoa ushauri na usimamizi wa ujenzi wa miradi hiyo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa  shirika lake lipo tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika usimamizi na kutoa ushauri wa ujenzi wa miradi ya viwanda vya kuzalisha sukari na kwamba walishatoa huduma kama hiyo katika nchi mbalimbali zikiwemo Brazil na Bolivia.

 

Jafo awapa tano watendaji Manispaa ya Kigamboni
Video: JPM afanya ziara ya kushtukiza kigamboni