Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amewapigia magoti Watanzania na kuwaomba waweze kukichangia chama chake ili waweze kufika katika mikoa 18 kwa lengo la kuzungumzia masuala ya ukiukwaji wa haki za wananchi na hali ngumu ya maisha.
Ameyasema hayo hii leo katika kampeni za uchaguzi wa udiwani katika Kata 43 zilizopo kwenye mikoa 18 chama chake cha ACT Wazalendo kimeweka wagombea katika Kata 28 na kwamba kupitia uchaguzi huo ndipo watakapopata nafasi ya kuwaamsha Watanzania kupitia kampeni kukataa uminywaji wa haki za binadamu na kutaka mabadiliko ya Sera za kiuchumi.
“Nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania wenye uchungu na Nchi yetu kuchangia kampeni zetu. Tunataka kufika kila ya nchi yetu na wewe ndio utatuwezesha kufika. Chochote ulicho nacho tunaomba utuchangie kwa kutumia namba hizi hapa,”amesema Kabwe
Hata hivyo, Zitto Kabwe yuko katika kampeni za udiwani huku akiwaomba Watanzania kukichangia chama hicho ili kiweze kufikia adhma ya kuleta maendeleo nchini.