Mwanasiasa Zitto Kabwe ameingilia kati Sakata la Kiungo kutoka Zanzibar Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye amegonga mwamba kwa mara ya pili, mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’.

Feisal aliomba kurejewa kwa maamuzi ya shauri lake dhidi ya Young Africans, lakini bado Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ikaendelea kusimamia msimamo wake wa kumtambua kama Mchezaji halali wa Klabu hiyo ya Jangwani.

Zotto Kambwe ambaye ni Kiongozi wa Chama cha Siasa cha ACT Wazalendo amesema kuna haja ya Shirikisho la Soka ‘TFF’ na Uongozi wa Young Africans kumaliza sakata hilo, ili kumpa uhuru Feisal wa kuendelea na maisha yake ya soka.

Amesema kinachofanyika hivi sasa ni kama kumlazimisha Mchezaji huyo kurejea kwenye klabu ambayo tayari ameshathibitisha hatoitumikia tena, jambo ambalo sio sahihi kwa maslahi ya pande zote mbili.

“Sijui Young Africans na TFF wanawaza nini. Kwani (Feisal Salum ) hawezi kupigwa faini kisha akaenda Timu atakayo? Ni lazima kumlazimisha kucheza timu ambayo hataki?” amesema Zitto Kambwe

Feisal alitangaza hadharani kuvunja mkataba na Young Africans mwishoni mwa mwaka 2022, lakini baadae Uongozi wa Klabu hiyo ulimshtaki TFF kwa kushinikiza arejee kambini kujiunga na wenzake lakini haikuwa hivyo.

Rais Mteule atoa wito kwa wapinzani
Anayesakwa kwa kumuua mkewe Moshi, amtumia ujumbe mama mkwe