Watu 32 wamefariki dunia na wengine 3 kujeruhiwa vibaya katika ajali mbaya iliyotokea leo Mei 6, 2017 katika mlima Rhotia kabla ya kuingia wilayani Karatu mkoani Arusha baada ya basi lililokuwa limemeba wanafunzi wa shule ya msingi ya Lucky Vicent waliokuwa wanaenda kufanya mashindano ya ujirani mwema Karatu kutumbukia kwenye korongo.

Athibitisha kutokea kwa ajali hiyo wakati akizungumza na Dar24, Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo amewataka madereva kuwa makini ikiwa ni pamoja na kufuata sheria zote wawapo barabarani kwani kipindi hiki siyo kizuri kutokana na hali ya mvua zinazoendelea kunyesha.

Kamanda Mkumbo amesema bado uchunguzi unaendelea kujua chanzo cha ajali hiyo iliyosababisha maumivu makubwa katika jamii kwani Wanafunzi 29 na Walimu 3 wamepoteza maisha, huku wengine 3 wakijeruhiwa vibaya.

Waziri Mwigulu, Zitto watoa pole vifo vya wanafunzi, walimu Arusha
Breaking: Wanafunzi 29, walimu 3 wapoteza maisha ajali ya basi Karatu