Moja kati ya habari ziliopewa nafasi na vyombo vya habari nchini ni mvutano kuhusu mwenendo wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania uliopelekea wabunge saba wa vyama vya upinzani kusimamiswa kushiriki shughuli za bunge kwa vipindi tofauti, akiwemo mbunge na Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe na wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Sakata hilo limeendelea ambapo leo chama cha ACT -Wazalendo kupitia Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano, Ado Shaibu wamejitokeza mbele ya wanahabari kueleza msimamo wa chama chao kuhusu sakata hilo.

Shaibu ameeleza kuwa chama hicho kimeandaa mapokezi ya kiongozi wao ambaye amekumbwa na adhabu hiyo mapokezi ambayo yamepangwa kufanyika Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa baada ya mapokezi hayo, utafanyika mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Zakhiem Mbagala, lengo likiwa ni kuwapa nafasi wabunge hao kueleza ukweli wa yale yanayoendelea bungeni Dodoma.

Katibu wa Itikadi mawasiliano na uenezi wa chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam

Pamoja na mandalizi hayo chama hicho kimewaandikia barua makatibu wa vyama vya upinzani ambao nao wanapinga adhabu hiyo kutoka CHADEMA, CUF,na NCCR-MAGEUZI kuwaomba kuungana nao katika mapokezi hayo ambayo yamepewa jina la ‘Oparesheni Linda Demokrasia’ na bado hawajapata majibu yao lakini wanaamini wataungana nao.

Alisema baada ya mkutano huo, watazunguka katika mikoa mingine minne kuungumza na Watanzania.

Polisi waitosa ahadi waliyompa Maalim Seif, alalama
Golden State Warriors Waanza Vyema Fainali Ya NBA