Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia Airtel money imedhamiria kuwakomboa Watanzania kwa kutoa ajira kwa kuanzisha ushirikiano wa uwekezaji na uendashaji wa maduka yake ya kisasa maarufu kama Airtel Money Branch.

Aidha, kwa wale ambao watapata fursa hiyo, kampuni ya Airtel itawawezesha kwa kuwapatia vifaa vyote muhimu ikiwemo kupiga chapa duka, floti kwenye akaunti ya Airtel Money pamoja na simu za kuendesha duka la Airtel Money kwa mafanikio.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Masoko na Uwekezaji wa Kampuni hiyo, Isack Nchuda wakati wa kutangaza ushirikiano wa uwekezaji huo, ambapo amesema kuwa Airtel ina nia ya dhati ya kuhakikisha Watanzania wanapata fursa ya kujiajiri kupitia Airtel Money.

Amesema kuwa Airtel Fursa mpaka sasa imewawezesha vijana wengi kuweza kujiajiri na kuweza kutimiza malengo yao ambayo wamekuwa wakiyatamani kwa muda mrefu katika maisha yao.

Vile vile hiyo Kampuni hiyo imekuwa na muendelezo wa kutoa fursa za kujiajiri kwa Watanzania, ambapo imeweza kufungua maduka ya huduma za simu mkononi nchini kote, ikiwa na lengo la kuendelea kuwawezesha vijana vijana kujiajiri.

“Tunaamini hii ni njia pekee ya kuwafikia wateja wetu na kujua changamoto zao na kuzitatua kwa wakati na vilevile kuwaunganisha na huduma na bidhaa zetu za kipekee na kibunifu zinazosaidia kutatua changamoto zao za kila siku za kijamii na kiuchumi,”amesema Nchuda

Hata hivyo, Maduka hayo yatatoa huduma mbalimbali zikiwemo huduma za kifedha, huduma za intaneti, kuongeza salio , kusajili namba na pia kuunganisha wateja wapya kwenye mtandao wa Airtel.

Kuanzishwa kwa maduka hayo sehemu mbalimbali nchini kunadhihirisha kuwa Airtel imeamua kuungana na serikali kuweza kuwekeza na kutoa ajira kwa Wtanzania nchini kote kwa ujumla.

Magazeti ya Tanzania leo Mei 10, 2018
Video: Kamwe serikali haitokubali kuchezewa na wafanyabiashara- Majaliwa