Maofisa watatu wa Kituo cha Uwekezaji nchini cha Tanzania Investment Center (TIC) wamefariki dunia katika  ajali mbaya ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia leo maeneo ya Chalinze wakiwa njiani kuelekea jijini Dodoma.

Waliofariki ni Saidi Amiri Moshi, Kaimu Mkurugenzi wa Research zamani Corporate Affairs, Zacharia Kingu (Kaimu Mkurugenzi wa Corporate Affairs zamani Investment Promotion) na Martin Masalu (Meneja Research).

Taarifa juu ya vifo hivyo imethibitishwa na mganga mkuu wa kituo cha Afya Msoga.

Waliopata majeraha ni wawili akiwemo Godfrey Kilolo, Meneja wa Sheria na dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina moja tu la Priscus.

Wote walikuwa wakielekea Dodoma kwa ajili ya mkutano ambao unatakiwa kufanyika leo Jumanne jijini humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo.

Dar24 inatoa pole kwa ndugu na jamaa wa karibu wa marehemu hawa Mungu azipumzishe roho zao kwa amani.

Machinga wapigwa marufuku barabara kuu
Magereza watoa msimamo Sugu kuvaa nembo ya mfungwa uraiani

Comments

comments