Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Olympic Lyon, Alexandre Lacazette amekamilisha vipimo vyake vya afya tayari kujiunga na Arsenal kwa ada ya  Pauni Milioni 52.
Lacazetti mwenye umri wa miaka 26, aliwasili kwenye uwanja wa mazoezi wa Arsenal jana  mchana na kuanza vipimo vya afya na anatarajiwa kukamilisha usajili wake hii leo.
Kwa kuanzia Arsenal itailipa Olympic Lyon Pauni Milioni 46 ambayo itaongezeka kwa Pauni Milioni 6 zaidi ili kumsajili mshambuliaji huyo mzaliwa wa Ufaransa.
Uhamisho huo utamfanya Lacazette kuwa mchezaji ghali zaidi Arsenal na kumpiku Mesut Ozil aliyenunuliwa kwa Paundi Milioni 42.5 mwaka 2013 akitokea Real Madrid.

?LIVE: Waziri Mkuu akitoa hotuba ya kuahirisha Bunge
Prof. Kabudi kuifuta rasmi TMAA