Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema wapo tayari kuingia hasara la kumuachia Alexis Sanchez kuondoka klabuni hapo kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu, lakini si kumuuza katika kipindi hiki ambacho kumekua na tetesi za usajili zinazomuhusu mshambliaji huyo kutoka nchini Chile.

Sanchez mwenye umri wa miaka 28, kwa sasa anahusishwa na taarifa za kuwindwa vikali na klabu tajiri ya jijini Paris nchini Ufaransa Paris St Germain, kufuatia mkanganyiko ulioibuka kati yake na Arsenal wa kutoafikiana kusaini mkataba mpya.

“Hakuna chochote kinachoendelea dhidi ya Sanchez,”  Alisema Wenger katika mkutano na waandishi wa habari uliokua unazungumzia mchezo wa ligi wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Stoke City.

” Sanchez kwa sasa anaelekea mwishoni mwa mkataba wake, amesaliwa na mwaka mmoja. Hakuna lolote linaloendelea katika mpango wa kumsainisha mkataba mpya.

“Hakuna kitakachotuzuia kuendelea kufanya nae kazi katika mwaka huo mmoja uliosalia kwenye mkataba wake, tukimalizana nae atakua huru kuondoka mwishoni mwa msimu huu.”

Katika hatua nyingine mzee huyo wa kifaransa amezungumzia maendeleo ya Sanchez, kwa kusema bado anaendelea kupata nafuu, baada ya kukabiliwa na maumivu ya misuli ya tumbo, na huenda akarudi uwanjani katika mchezo wa ligi ya England dhidi ya Liverpool, tarehe 27 mwezi huu.

Wakati huo huo Wenger amesema hakuna mazungumzo yoyote yanayoendelea kati ya viongozi wa klabu ya Arsenal na viungo Jack Wilshere na Alex Oxlade-Chamberlain, ambao pia wamesaliwa na mikataba wa mwaka mmoja kila mmoja.

Andres Iniesta Kuikosa Real Madrid
Majaliwa amtaka balozi kuimarisha uhusiano wa Kidplomasia