Hatimaye King Kiba ameachia kwa mkupuo audio na video ya wimbo wake mpya alioubatiza jina la ‘Mvumo wa Radi’.

Kiba amerejea mikononi mwa Man Walter na kupika pamoja ‘jiwe’ linalokuwa la kwanza kutoka kwake tangu afunge pingu za maisha.
Ametumia video ya wimbo huo pia kusogeza kinywaji chake kwa mashabiki wake, kuonesha hivi sasa ni muziki, biashara na ubalozi wa nguvu.

Ni dhahiri kuwa video ya wimbo huu huenda itavunja rekodi ya kutazamwa mara nyingi kwani ndani ya dakika chache tangu atangaze kuwa ameiweka rasmi kwenye YouTube, views zinaongezeka kwa kasi ya mshale wa saa.

Endelea kusubiri ripoti ya kinachojiri kuhusu video hii pamoja na uchambuzi wake, hapa Dar24.

Mbunge wa Shinyanga Mjini alamba dili Bunge la Afrika
Msichana aliyemuua mumewe aliyekuwa anambaka ahukumiwa kifo

Comments

comments