Papa Mtakatifu Francis amemteua Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi kuwa Askofu Mkuu Mwandamizi kurithi Jimbo kuu la Dar es Salaam, Tanzania na kuchukua nafasi ya Polycarp Pengo.

Katika barua iliyotolewa na Katibu Mkuu TEC, Raymond  Saba kwamba Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Yuda Thaddeus Ruwaichi alikuwa ni Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza, Tanzania.

Tarehe 15 Januari 2005, Mtakatifu Yohane Paulo II alimteuwa Askofu Ruwaichi kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Dodoma na kusimikwa rasmi tarehe 19 Februari 2005

Hata hivyo 2011 Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza na kusimikwa rasmi tarehe 9 Januari.

Mabingwa wa soka Italia wamnyakua Emre Can
P - Funk awapa nondo wasanii wa Bongo Fleva, ‘usikurupuke’

Comments

comments