klabu ya Azam FC, imetoa kipigo kikubwa cha mabao 5-0 dhidi ya timu ya Shupavu FC ya mkoani Morogoro kwenye mchezo uliochezwa hapo jana.

Azam ambayo imekuwa na utamaduni wa kuwaamini vijana katika kikosi cha kwanza imeshuhudiwa nyota wake chipukizi wa timu hiyo, Paul Peter akiibuka shujaa baada ya kufunga mabao matatu (Hat-trick) katika ushindi huo.

Aidha, Peter amefunga mabao hayo katika kipindi cha pili akiwa ameingia kuchukua nafasi ya mshambuliaji Mbaraka Yusuf. ambapo alifunga katika dakika za 52, 77 na 88.

Matokeo hayo sasa yanaifanya Azam itinge hatua ya 16 bora ya michuano hiyo ya Shirikisho Tanzania (FA) ambapo sasa itasubiri mechi zingine za zimalizike kabla ya droo kuchezeshwa na kujua watakutana na timu gani.

Hata hivyo, Mabao mengine ya Azam FC yamefungwa na nyota wengine Yahya Zayid dakika ya 45 huku Iddi Kipagwile akifunga bao la pili kwenye dakika za majeruhi kipindi cha kwanza.

 

Wapinzani wagoma kutoa maoni Bungeni
Magazeti ya Tanzania leo Januari 31, 2018