Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa Bafetimbi Gomis ameondoka Swansea City na kutimkia Galatasaray ya Uturuki kwa ada ya uhamisho iliyofanywa siri baina ya klabu hizo.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, alisajiliwa na Swansea City mwaka 2014 akiwa mchezaji huru, na amefanikiwa kuifungia klabu hiyo mabao 13 katika ligi ya nchini England kabla ya kupelekwa kwa mkopo Olympic Marseille, ambapo alifunga mabao 21 katika michezo 34 aliyocheza.

“Swansea City tumekubaliana na Galatasaray kukamilisha uhamisho wa Bafetimbi Gomis, na makubaliano yetu yataendelea kuwa siri kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa baina yetu,” Swansea City wamethibitisha kupitia tovuti yao. (www.swanseacity.com)

“Kila mmoja klabuni hapa anamshukuru Bafetimbi kwa kazi nzuri aliyoifanya tangu mwaka 2014, na tutaendelea kuukumbuka mchango wake.”

Trump atoa masharti mapya kwa nchi za Kiarabu kuingia Marekani
Makonda awatoa dinner WCB