Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC imesema kuwa haihitaji wasimamizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya wala kutoka Barani Afrika.

Imesema kuwa Umoja wa Mataifa, Afrika Kusini, Umoja wa Ulaya na wengine, haihitaji msaada wao, washauri wao wala maoni yao kuhusu maandalizi ya uchaguzi uliopangawa kufanyika Desemba 23 mwaka huu.

Aidha, Jumatatu iliyopita viongozi jijini Kinshasa walipinga ripoti iliyotangazwa na vyombo vya habari, bila ya kuthibitishwa na serikali kuhusu kuteuliwa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki kuwa mjumbe maalumu wa uchaguzi ujao wa nchi hiyo.

“Nawaambieni kwamba hakutokuwepo tena na mjumbe maalum yeyote katika nchi hii ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, hata kama ni Thabo Mbeki,”amesema mshauri wa masuala ya Kidemokrasia wa rais Kabila, Barnabe Kikaya Bin Karubi

Hata hivyo, msimamo wa serikali ya Kinshasa dhidi ya wasimamizi wa Umoja wa mataifa, Umoja wa Ulaya na Afrika Kusini unaangaliwa kwa jicho la wasi wasi na wanadiplomasia.

 

Lema: Suala la haki, usawa na utawala wa sheria sio la Chadema peke yake
Barabara ya chini ya Ardhi ya kusafirisha dawa za kulevya yagundulika