Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, azidi kuja juu baada ya kuendelea kuzitangaza bidhaa zake, Diamond Karanga na Chibu Perfume nchini Rwanda.

Ambapo mwishoni mwa wiki hii alikuwa nchini humo na ameeleza kuwa hivi karibuni ana mipango mikubwa na bidhaa hizo kwa upande wa uwekezaji ambapo amesema mipango yake ni kujenga kiwanda cha Diamond karanga nchini Rwanda.

Diamond anaamini kuwa endapo mpango huo utakamilika, kiwanda hiko kitatoa fursa za ajira na kwamba lengo la biashara yake ni zaidi ya kupata soko nchini humo.

‘Nitafurahi zaidi kama watu watafurahia bidhaa zangu, lakini zaidi wakipata ajira na kubadili hali ya kimaisha” amesema Diamond Platinumz.

Hata hivyo ameeleza kuwa wasanii wanapaswa kufanya muziki si tu kuburudisha, lakini pia uwe ni chanzo cha biashara inayoweza kuwanufaisha watu wengi.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Diamond amepost picha akiwa na wasanii wa Rwanda wakipata Dinner na kushare experience kuhusu muziki.

”Last night during my Dinner with my Fellow Artists from #Rwanda! It was a great evening, sharing experiences and ideas….Time to put our East African / African industry on the global map! Let’s do it, fam….✊” – Diamond Platnumz

 

Ziara ya Majaliwa yang'oa kigogo Mara
Netanyahu amshukuru Trump kwa maamuzi ya Kihistoria