Wanasheria kutoka Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwa pamoja wamemchagua Wakili, Fatma Karume kuwa rais mpya atakaye kiongoza Chama hicho.

Aidha, Fatma Karume anachukua nafasi ya mwanasheria mwenzake, Tundu Lissu ambaye anamaliza muda wake Kikatiba.

Katika uchaguzi huo uliofanyika hii leo jijini Arusha, Dkt. Rugemeleza Nshala amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa TLS.

Kwa mujibu wa katiba ya chama hicho cha wanasheria, uongozi ndani ya chama hicho hudumu kwa muda wa mwaka mmoja.

 

Wananchi Makowo wajenga kituo cha afya
Baba wa mtoto mwenye asili ya China kutafutwa

Comments

comments