Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ameutaka uongozi wa klabu ya Yanga kutoa jibu linaloeleweka kabla ya siku ya leo Jumapili juu ya kujitoa kwao kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, (CECAFA KAGAME CUP).

Karia ameyasema hayo baada ya Yanga kuiandikia barua TFF kuwaarifu kutoshiriki michuano hiyo kutokana na kubanwa na ratiba ya mashindano mengine.

Amesema kuwa amelazimika kutoa agizo hilo kutokana na kutoridhishwa na sababu walizozitoa Yanga kwani hata timu nyingine zinazoshiriki michuano hiyo zina ratiba ngumu pia.

“Kabla hata hatujalipeleka suala hili CECAFA, nauomba uongozi wa Yanga hadi leo jumapili uwe umetoa jibu la kueleweka juu ya mashindano hayo,”amesema Karia.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kwenye CECAFA KAGAME CUP kuna timu za Gor Mahia na Simba ambazo pia bado ziko kwenye michuano ya SportsPesa Super Cup hivyo kama kulalamikia ratiba zenyewe zingekuwa za kwanza kufanya hivyo.

 

Video: Harmorapa afunguka kutoswa na Meneja wake
Simba, Gor Mahia nani kwenda Goodison Park?

Comments

comments