Miss Tanzania 2006, Wema Isaack Sepetu leo hii ilikuwa siku yake ya kusomewa hukumu kufuatia kesi iliyokuwa inamkabili ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya bangi.

Hivyo leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imehairisha kumsomea hukumu hiyo mpaka ijumaa ya Julai 20, 2018 kutokana na sababu za kiuchunguzi kama ambavyo ameeleza Wema Sepetu mara baaada ya kutoka Mahakamani.

”Mpaka Ijumaa ndio watatoa hukumu, Hakimu amesema kuna vitu ambavyo alikuwa anatakiwa kuvifanyia ‘research’ kwa undani zaidi, kwahiyo wamesema mpaka ijumaa ndio itatolewa hukumu”.

Aidha mnamo April 23, 2018 Wema Sepetu na wafanyakazi wake wawili walikutwa na kesi ya kujibu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na kukabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya bangi.

 

 

 

Sunday Oliseh: Ufaransa imeitumia Afrika kupata Kombe la Dunia
Mbarawa amtumbua mkurugenzi mamlaka ya maji Kigoma

Comments

comments