Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameitakia heri timu ya Yanga katika mchezo wao wa kwanza wa fainali wa Kombe la Shirikisho Afrika unaochezwa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam

Chongolo ameitakia heri ya ushindi timu hiyo leo May 28, 2023 wakati akizungumza katika mkutano na wananchi wa Kata ya Malangali, Jimbo la Mufindi Kusini.

Chongolo yupo Mkoani Iringa kwa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, pamoja na kuhimiza uhai wa chama ngazi za mashina, na kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 29, 2023
Aliyempiga mke wake na kumng’oa jino akamatwa