Waziri wa Maliasili, Hamisi Kigwangalla amechukuliwa na helkopta na kusafirishwa hadi Kilimanjaro katika hospitali ya KCMC kwa ajili ya matibabu zaidi.

Kigwangalla leo Jumamosi Agosti 4, 2018 amepata ajali eneo la Magugu mkoani Manyara na kupata majeraha sehemu mbalimbali mwilini.

katika gari hilo alikuwepo Dk Kigwangalla, dereva wake, mwandishi wa habari, msaidizi wake na mlinzi ambapo ofisa habari wa wizara hiyo, Hamza Temba amefariki dunia ameripoti kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Augostino Senga

Hapo awali Waziri Kigwangalla alikuwa akipatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Magugu.

Dk Kigwangalla ana maumivu katika mbavu, kiuno na hawezi kutembea.

Aidha hali ya waziri huyo inaendelea vizuri licha ya kuwa ameumia mkono wa kulia, kifua na shingo.

Gari alilopatia ajali Waziri wa Maliasili, Dk. Hamis Kigwangalla.

NEC yatangaza tarehe ya uchaguzi majimbo ya Ukonga, Korogwe na Monduli
Maswali 10 yanayoulizwa mara kwa mara kwenye 'Interview'