Nyota wa muziki wa bongo fleva kutoka lebel ya ‘WCB’, Harmonize ameweka rekodi yakipekee kwa wimbo wake wa ‘Kwa Ngwaru’ kuwa wimbo wa kwanza kutoka Africa Mashariki kufikisha watazamaji ‘Views’ milioni 10 ndani ya mwezi mmoja kwenye mtandao wa YouTube.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ameandika ‘This is the firts East African music video to reach 10 milion viewers in just one Month’ akimaanisha hii ni mara ya kwanza kwa wimbo wa Afrika Mashariki kufikisha watazamaji milioni kuni ndani ya mwezi mmoja.

Kwa Ngwaru ni wimbo ambao Harmonize amefanya na Diamond Platnumz ukiwa ni wimbo wa pili kufanya na Diamond baada ya wimbo unaoitwa ‘Bado’ uliotoka miaka miwili iyopita.

 

Hii ndo timu atayohamia Lionel Messi akiondoka Barcelona
Kikwete atoa neno la hisia kwa Rais Magufuli, Kinana na Bashiru

Comments

comments