Kijana Reza Parastesh, raia wa Iran amenusurika kutupwa mahabusu kwa kusababisha taharuki mitaani.

Reza, ambaye ni mwanafunzi, pamoja na kuwa shabiki mkubwa wa mchezaji wa Barcelona Lionel Messi, pia anafanana naye kwa muonekano. Ikiwa ni namna ya kuonyesha mapenzi yake kwa nguli wake huyo, Reza amekuwa ananyoa nywele na hata kufuga ndevu kama Messi halisi.

Video: Magari matano yenye kasi ZAIDI duniani (S01E01)

Bila kujiuliza kama anayepita katika mitaa ya mjini wa Hamedan uliopo magharibi ya Iran si Messi halisi, makundi ya watu walianza kumfuata Reza kila anakokwenda ili wapige naye picha hali iliyosababisha msongamano na vurugu.

Polisi walilazimika kumwondoa Reza kutoka kwenye eneo lenye vurugu kwa usalama wake na raia waliokuwepo mahali hapo. Polisi wamempa onyo kuwa endapo hali hiyo itatokea tena basi hawatasita kumchukulia hatua za kisheria kwa kusababisha vurugu.

Tanzania na Afrika Kusini kuweka mikakati ya pamoja ya kukuza uchumi
JPM awalilia wanafunzi, asema tumewapoteza mashujaa wetu katika elimu

Comments

comments