Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Ilala, Kamanda Mwashishanga Mwanambiti amesema kuwa hadi sasa wamewakamata madereva watano wa Serikali kwa matumizi mabaya ya barabara za mwendo kasi.

Kamanda huyo amesema kuwa hata leo asubuhi wamesimamisha baadhi ya viongozi na kuwaagiza madereva wao wawapeleke ofisini kisha warudishe magari hayo polisi baada ya kukiuka sheria za barabarani.

Amesema kuwa hadi sasa kuna madereva wa Serikali ambao wapo wamefungiwa na wapo mahabusu mara baada ya kukamilisha ushahidi watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Aidha, Kamanda huyo amewaomba viongozi kutowaruhusu madereva wao kupita katika barabara za mwendo kasi au kuvunja sheria zozote za barabarani kwani jeshi hilo halitasita kuwachukulia hatua za kisheria.

Makonda atoa shehena ya mifuko 1,200 ya saruji kwa Askari 12 bora
Anaswa kwa kumuua rapa wa Marekani