Ni kawaida kwa nyumba za vijijini na maeneo yaliyo na ardhi ya kutosha kuwa na eneo linaloitwa jalalani ambalo wakazi hutupa taka, mara nyingi huwa ni shimo refu kiasi ambalo hata kama limejaa kuna baadhi ya familia ambazo sio wastaarabu huendelea kutupa taka.

Lakini maeneo ya mijini na hasa yale ambayo nyumba zimebanana huwa na vifaa maalumu vya kuhifdhia taka kama vile katika viroba ambavyo vikijaa wanavibeba na kwenda kutupa mahali husika au kusubiri gari la kuzoa taka.

Haijalishi nyumba ina jalala au inategemea gari la kukusanya taka, suala la kuwa na ‘dustbin’ dogo ndani ya nyumba linafaa kwa wote, kwaajili ya taka ndogo ndogo kama vile maganda ya viberiti, sabuni zakuogea, tishu ambavyo vinahitaji kuchomwa baadaye au kutupwa nje.

Hivyo ni muhimu ndani ya nyumba kuwa na vifaa maalumu kwaajili ya kuhifadhi taka ndogo na kavu ili kuweka nyumba katika hali ya unadhifu, siyo maeneo yote yanatakiwa kuwanacho, haya ndiyo maeneo matatu muhimu.

Chumba cha kulala

Hiki kinatakiwa kuwa na chombo kwaajili ya kuweka taka ndogo zinazo zalishwa chumbani ambacho kinaweza kukaa, pembeni ya kabati au mlango lakini kama chumba kina choo ndani chenye nafasi kinaweza kuwekwa chooni.

Sebuleni au ukumbini

Sehemu hii inapaswa kuwa na kifaa hiki cha kuhifadhia uchafu unaozaishwa na kukusanywa kama vile visoda vinavyobakia baada ya kufungua vinywaji, tishu zinazotumika na pia ni muhimu kikakaa kwenye kona ya mlango wa kutokea.

Jikoni

Jikoni pia kunauhitaji wa kuwa nakifaa kidogo cha kuhifadhia taka ambazo huzalishwa wakati wa kupika, kifaa kinachowekwa jikoni kinatakiwa kiwekewe mfuko wa ambao haupitishi maji kwasababu taka zake nyingi ni mbichi.

Hata hivyo inashauriwa pia nyumba iwe na buni ya kuchomea taka iliyojengwa kitaalamu ambayo inazuia moshi mchafu usizagae katika anga na kuchafua hali ya hewa.

Aidha faida nyingine ya kuwa na kifaa kidogo cha kuhifadhia taka ndani ya nyumba ni kusaidia watoto kuwa na mazoea ya kuweka nyumba katika hali ya usafi na kutotopa taka kiholela hata wanapokuwa nje ya nyumba.

Mabeste: Niliposikiliza wimbo wa Stamina nilicheka, nina nyimbo kama hizo lakini…
Fanya haya kulinda meno ya watoto kutoboka, kuoza

Comments

comments