Mchekeshaji maarufu nchini Amri Athumani maarufu kama Mzee Majuto, amerejea nchini kutoka India alikokuwa akifanyiwa matibabu ya tezi dume.

Ambapo amefunguka kuwa sasa anaendelea vizuri mara baada ya kupatiwa matibabu ya hali ya juu amesema kuwa endapo asingefanyiwa matibabu hayo huenda angepoteza maisha.

”Mimi sijambo nashukuru, Hospitali ni Hospitali isipokuwa wenzetu wapo mbali zaidi, nimefanyiwa mambo mengi sana ambayo kama nisingefanyiwa ningeondoka mapema sana namshukuru Mungu” amesema Majuto.

Mzee Majuto ameongeza kuwa baada ya kumaliza matibabu hayo anataka kutenga muda mwingi kwaajili ya kupumzika zaidi na kuacha kujihusisha na masuala ya sanaa ya uchekeshaji na kudai kuwa Tanzania bado kunawachekeshaji wengi ambao wataweza kuendeleza sanaa hiyo.

Muigizaji huyo wa vichekesho kwasasa amepokelewa na yupo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mei 4, 2018 Mzee Majuto alisafirishwa kwa gharama za serikali, kwenda nchini India kwa matibabu ya tezi dume baada ya kusumbuliwa na ugonjwa huo kwa kipindi cha muda mrefu.

Video: Lembeli aivuruga CCM, Bashiru-Ruksa wabunge wa CCM kuikosoa Serikali
Video: LHRC yalia na katiba mpya, Bisimba afunguka haya