Ushirikiano kati ya Marekani na Uturuki unaendelea kuimarika nchini Syria, pamoja na kuwepo mgogoro wa mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa Jeshi la Uturuki, nchi hizo mbili ambazo ni washirika wa Umoja wa Kujihami wa Ulaya (NATO) wana karibia kuanza kufanya ulinzi wa doria ya kijeshi wa pamoja katika mkoa wa Manbij kaskazini mwa Syria.

“Ingawaje zoezi hilo limechelewa kwa siku chache kwa mujibu wa ratiba, mpangilio huo unaendelea bila ya kizuizi chochote. hivi sasa tunaanza kipindi cha ulinzi wa doria ya pamoja,”amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu

Aidha, mji wa Manbij umeendelea kuwa ni sehemu yenye mvutano katika mahusiano yaliyoko kati ya Marekani na Uturuki tangu wapiganaji wa Syrian Democratic Forces (SDF) walipouteka mji huo uliokuwa mikononi mwa kikundi cha Islamic State.

Hata hivyo, sehemu kubwa ya kikundi cha SDF kinawapiganaji wa kikundi cha wanamgambo wa Kikurdi wa Syria, na kikundi cha YPG ambacho kimetajwa kuwa ni magaidi na Ankara kikiwa na mafungamano na chama cha PKK.

Jeshi la Polisi nchini Uganda lakamata waandamanaji 103
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 21, 2018