Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha, imempandisha kizimbani mkazi wa kijiji cha kikatiti, Warieli Mungure, kwa tuhuma za kuuza gongo na kutaka kumpa rushwa Mkuu wa kituo cha Polisi cha kikatiti.

Naibu mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha, Frida Wikesi ametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa mtuhumiwa huyo alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo kusomewa shtaka Octoba 10 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo awali TAKUKURU wilaya ya Arumeru, alipata  taarifa kutoka kwa Mkuu wa kituo cha Polisi aliyeeleza kuwa Mungure alimuahidi kumpatia kisi cha shilingi 100,000 kila mwezi ili asifuatiliwe katika biashara yake haramu ya kuuza gongo.

Baada ya kupata taarifa hizo za awali walianzisha uchunguzi wa awali na baada ya kuthibitisha tuhuma hizo, waliandaa mtego uliofanikisha kumkamata Mngure Oktoba 9 Mwaka huu katika eneo la Enspall Lodge, Kikatiti kwa kwenda kinyume na kifungu cha 15 (1) (b) na (2) cha sharia namba 11 ya mwaka 2007.

Takukuru imetoa wito viongozi na watu wengine kuiga mfano wa mkuu huyo wa kituo cha polisi ambaye hakuwa tayari kuhongwa na alatekeleza wajibu na kutunza Uzalendo.

 

Jermaine Dupri atoa mtazamo tofauti kwenye fainal za Super Bowl
RC Mwanri aunguruma jijini Dar, asema hata jirani 'Sukuma ndani'

Comments

comments