Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga amepiga marufuku uzinduzi wa filamu ya Magwangala iliyokuwa inatarajiwa kuzinduliwa na Naibu Waziri wa Habari kwa madai kuwa ina maudhui ya kuutia doa mgodi wa dhahabu wa Geita Gold Mine (GGM) uliopo mkoani humo.

Akizungumzia hatua hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Geita mjini amesema kuwa hatua hiyo imekuja mara baada ya kupokea malalamiko kutoka katika mgodi huo kuwa filamu hiyo inagusa maslahi na kuchafua taswira ya mgodi huo.

Aidha, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Anastazia Wambura ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu hiyo uliopigwa marufuku na mkuu huo,, amesema kuwa GGM walitishia kwenda mahakamani kama uzinduzi wa filamu hiyo ungefanyika.

“Nilifika kwa mkuu wa mkoa kama mwenyeji wangu, ndipo nikapata taarifa kuwa GGM wamepeleka malalamiko kuhusu filamu hiyo kuwa inagusa maslahi ya mgodi huo, hivyo kama itazinduliwa basi wao wataenda mahakamani,”amesema Wambura

Hata hivyo, Filamu hiyo ambayo ilikuwa inatarajiwa kuzinduliwa na Naibu Waziri huyo inaelezea maisha ya wachimbaji wadogo wadogo wanavyopata shida na kutegemea Magwangala katika mgodi huo.

 

Sakaya amshukia Maalim Seif, ahofia uwezo wake wa kufikiri
Mpina anena mazito kuhusu wakuu wa mikoa na wilaya