Mwanasiasa kutoka muungano wa upinzani nchini Zimbabwe MDC, Tendai Biti amenyimwa hifadhi ya kisiasa nchini Zambia

Jeshi la Polisi nchini Zimbabwe linamlaumu mwanasiasa huyo kwa kuchochea ghasia kufuatia uchaguzi wa wiki iliyopita ambapo alimtangaza Nelson Chamisa kutoka MDC kuwa ameshinda katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Waziri wa mambo ya nje wa Zambia amesema kuwa mwanasiasa huyo kutoka chama cha upinzani cha MDC hakuwa na sifa za kupewa hifadhi nchini Zambia.

Aidha, taarifa kutoka jeshi la polisi Zambia zinazo sambaa kwenye mitandao ya kijamii zinasema kuwa maafisa wa jeshi la polisi Zimbabwe walijaribu kumkamata mwanasiasa huyo.

Hata hivyo, kulikuwa na matumaini kuwa uchaguzi wa mwezi Julai mwaka huu ungeleta mabadiliko makubwa baada ya kumalizika kwa utawala wa Rais Robert Mugabe.

Mambo 5 usiyotakiwa kufanya mara baada ya kula
Tanzania yaandika historia Mkutano wa Kimataifa wa Manunuzi

Comments

comments