Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Alliance Schools utakaopigwa jijini Mwanza Ijumaa ya wiki hii timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani jijini Dar es salaam imepata pigo baada ya  mchezaji wao Mapinduzi Balama kulazimika kukaa nje ya uwanja.
Taarifa zimesema kuwa Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amethibitisha kwamba Balama atakuwa nje ya kikosi sababu ya majeraha.
Balama atakuwa nje ya mchezo huo kufuatia kuumia nyonga katika mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya JKT Tanzania.
Leo alfajiri kikosi cha Yanga kimeanza safari ya kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya mechi hiyo ambayo itakuwa ya aina yake kufuatia Alliance kuchapwa kipigo cha mabao 5-0 dhidi ya Azam FC juzi.
Mwakinyo, Mfilipino wapima uzito, tofauti yaonekana
Maeneo ambayo upinzani umeshinda Uchaguzi serikali za mitaa yawekwa wazi

Comments

comments