Mbunge wa Jimbo la Mtama kupitia tiketi ya (CCM) Nape Nnauye amesema kuwa hivi sasa kwenye sekta ya mifugo hali imekuwa mbaya zaidi ukilinganisha na kipindi cha nyuma na kudai kuwa alitegemea mabadiliko makubwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Ameyasema hayo bungeni wakati akichangia hoja ya taarifa ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji iliyowasilishwa bungeni, mjini Dodoma ambapo mbunge huyo amesema kitendo cha kufunikwa funikwa matatizo ya sekta hiyo ni kutoa kafara kwa wananchi zaidi ya asilimia 50 ambao wanategemea sekta ya mifugo.

“Hali inayoendelea kwenye sekta hii ya mifugo ni mbaya sana na kwa bahati mbaya kwa miaka sasa limekuwa linakuja na kuzungumzwa hapa bungeni moto unawaka halafu zinakuchukuliwa hatua za kufunika ule moto watu wananyamaza halafu dhuruma na hujuma zinaendelea pale pale,” amesema Nape

Hata hivyo, ameongeza kuwa kama serikali itaendelea na hatua hizo za zima moto kila unapowaka maana yake ni kuwatoa kafala asilimia 50% ya population ya nchi ya Tanzania ambayo inahudumiwa na sekta ya mifugo na kuwaacha na hali yao ikiwa mbaya zaidi.

Ujerumani kuunda serikali ya mseto
Magazeti ya Tanzania leo Februari 8, 2018