Siku kadhaa baada ya baadhi ya wasanii na wadau wa muziki nchini kuchanga fedha na kufanikisha kumpeleka katika nyumba ya uangalizi maalum (rehab), rapa mkongwe anayefahamika kam ‘Fanani’, kutokana na kuathirika na  matumizi ya dawa za kulevya, wasanii waliomtembelea wameelezea hali yake ilivyo hivi sasa.

Fanani ambaye alikuwa mmoja kati ya wasanii watatu waliokuwa wakiunda Hard Blasters Crew (HBC) miaka ya 90 akiwa pamoja na Profesa Jay na Big Willy, alikumbwa na jinamizi la matumizi ya dawa za kulevya kwa muda mrefu.

Rapa Nash MC ambaye hivi karibuni alitangaza kumshirikisha Fanani kwenye wimbo wake mpya na kupelekea kuzaliwa kwa wazo la kumchangia msanii huyo amekiambia kipindi cha Ladha3600 cha E-Fm kuwa hivi karibuni amemtembelea rapa huyo huko ‘Sober House’ na yuko katika hali nzuri.

Fanani na Nash MC

Fanani na Nash MC

“Watu ambao wako kule sober house wapo wengi na wanahudumiwa vizuri sana. Kwahiyo kwa sasa hivi mimi nataka kuwaambia kwamba tujitahidi pia kwenda kumtembelea, tusiishie kuchanga tu japo pia ni jambo zuri,” Nash alifunguka.

Nash MC aliwashukuru wadau wote waliomchangia Fanani na kuwezesha kutunzwa ndani ya jumba hilo akipatiwa matibabu. Alisema kilichofanywa na wadau hao ni tendo jema na mfano wa kuigwa.

BARAZA LA BIASHARA LAANDAA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA INDIA
Diva awacharukia Billnas Na Linah, amtumbua Billnas kwenye wimbo wake