Uongozi wa klabu ya Yanga, Kampuni ya GSM leo wamefanya oparesheni rasmi ya kutokomeza jezi feki zinazouzwa maduka mbalimbali hapa mjini na kusema kuwa watu wote wanaouza jezi feki wanahujumu timu ya Yanga na kufanya washindwe kulipa madeni yanayowakabili.

Ambapo leo wakiongozwa na Afisa mhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz wamepita maduka mbalimbali ya karikaoo na kukamata jezi feke.

“Hii tumeifanya leo pale Kariakoo mtaa wa Aggrey na Congo, baada ya kupata taarifa nikiwa ofisini na nilipigiwa simu na maintelijensia wa Yanga. Tumefanikiwa kukamata jezi feki za msimu huu na zile za zamani na mwenye duka ameonesha ushirikiano na sisi”, amesema Antonio Nugaz.

Amesema kuwa GSM pekee ndio wenye mamlaka ya kuuza, kuchapisha, na kutoa jezi zote kwa ajili ya msimu huu wa 2019/2020 hivyo amewaomba mashabiki kuwaunga mkono kwa kununu jezi orijino.

”Kama hanunui, hauzi maana hauitakii mema timu ya yanga kwamba anaihujumu Yanga, shabiki wayanga ambaye hununui original ujue unaihujuu timu yake, watu wanadai madeni yao hatulipi kumbe wajanja wanachukua hela tu”. amesema Antonio Nugaz

Aidha amewaomba wanachama na mashabiki wa Yanga kununua jezi ‘original’ za Yanga, ameongezea kuwa jezi ya Yanga haitandikwi chini wala haitundikwi kwenye mti.

Msemaji wa Yanga amesema zoezi hilo litakuwa endelevu nchini ili kuhakikisha klabu inafaidika kutoka kwenye mauzo ya jezi halisi zinazozalishwa na kampuni iliyopewa kazi hiyo.

Video: Ebitoke afunguka sababu za kumvamia Mlela, aanika siri ya nyuma ya pazia
Sababu ya mama kumzika mwanaye akiwa hai

Comments

comments