Wakati Serikali nchini Uganda ikijitahidi kupata njia madhubuti ya kukabiliana na uvamizi wa nzige wa jangwani, wakazi wa Kitgum nchini humo wanawakamata nzige hao na kuwafanya chakula.

Nzige wa jangwani walivamia vijiji vya Gogo na Abudere Februari 18, 2020 jioni na kukaa kwenye eneo la zaidi ya Kilomita tatu. Wakazi waliitumia siku hiyo na kesho yake kuokota nzige hao kwa chakula.

Kutansia Anena (60), amesema Nzige wamekuwa chakula tangu zamani na pia alilazimika kuwapata ili waongeze lishe yake kwa sababu ya uhaba wa chakula kutokana na mavuno duni mwaka jana.

Serikali imeanza kunyunyizia dawa ili kukabiliana na nzige hao. Wananchi wameonywa kuwakamata nzige kutoka maeneo ambayo yamepigwa dawa kwani kemikali hiyo ni hatari kwa mwili wa binadamu.

Kichina kuanza kufundishwa Sekondari
Siku tatu za uboreshaji daftari la wapiga kura Dar

Comments

comments