Imethibitishwa kuwa Kobe Bryant aliyefariki dunia katika ajali ya helikopta alikuwa na watu wanane akiwemo mwanaye, idadi ambayo ni zaidi ya iliyoripotiwa awali kuwa ni jumla ya watu watano.

US Today na CBS ni miongoni mwa vyombo vya habari vilivyoripoti kuhusu kuthibitishwa kwa taarifa za vifo vya watu tisa waliokuwa kwenye chombo hicho, Jumapili, Januari 26, 2020.

Vyombo vya usalama na Mamlaka ya Manispaa ya Calabasas vimeeleza kuwa ndege hiyo ilianguka majira ya saa nne asubuhi, baada ya kugonga ukingo wa mlima na kushika moto.

Waliofariki pamoja na nyota huyo ni wafuatao:

  1. Gianna Bryant- Mtoto wa Kobe Bryant
  2. John Altobelli- Baba yake Alyssa
  3. Keri Altobelli- Mama yake Alyssa
  4. Alyssa Altobelli- mchezaji mwenza wa Gianna Bryant
  5. Christina Mauser- Kocha wa mpira wa kikapu
  6. Sarah Chester- Mama yake Payton
  7. Payton Chester- Mchezaji mwenza wa Gianna
  8. Bryant Ara Zobayan-  Rubani.

Viongozi wa Marekani akiwemo Rais Donald Trump, Rais mstaafu, Barack Obama na watu wengine maarufu; na mashabiki wa mpira wa kikapu duniani kote wameomboleza tukio hilo, wakiandika jumbe mbalimbali za salamu za rambirambi kwenye mitandao ya kijamii.

Ripoti zilieleza kuwa walikuwa wanasafiri, Bryant akiwasindikiza kwenda kucheza mpira wa kikapu.

Bryant aliichezea Lakers ya Los Angeles kwa kipindi chote alichocheza ligi ya NBA, ikiwa ni tangu mwaka 1996 hadi 2016 na alifanikiwa kuisaidia kushinda mataji matano ya ubingwa wa NBA.

Mafuriko Lindi: wananchi 4500 waokolewa kwa boti
Kipa Yanga: "Simba walinifuata, nitafute kadi ya njano, wanipe IST mpya"

Comments

comments