Idara ya habari na mawasiliano ya klabu ya Simba imethibitisha kuwasili kwa kocha kutoka nchini Ufaransa Pierre Lechantre, anaechukua nafasi ya Joseph Omog aliyetimuliwa klabuni hapo mwishoni mwa mwaka jana, baada ya kupoteza mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Green Warriors.

Muda mchache uliopita mkuu wa idara hiyo Haji Manara, amethibitisha kupitia barua iliyosambazwa kwa njia ya mitandao ya kijamii ambayo inathibitisha kuwasili kwa kocha huyo.

Barua ya Manara inasomeka kama ifuatavyo.

Simba Sports Club

Dar es salaam

18/01/2018.

 

TAARIFA KWA UMMA

 Klabu ya Simba inayo furaha kubwa kuwajulisha Wanachama na washabiki wake kwamba imempata kocha wake mkuu mpya,Mfaransa Pierre Lechantre.

Kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo

Kocha Lichantre keshawahi kufundisha vilabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroun kilichotwaa ubingwa wa Africa 2000.

Kocha huyo pia alipata kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 na pia barani Asia mwaka 2012.

Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi

Na leo jioni kocha Lechantre ataishuhudia Simba ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa.

IMETOLEWA NA

HAJI S MANARA

MKUU WA HABARI SIMBA SC

SIMBA SC NGUVU MOJA

 

Mambosasa akanusha agizo la vimini na viduku
Viongozi Chadema watiwa mbaroni kuhusika na tukio la moto