Katika kuhakikisha kuwa Sekta ya Utalii nchini inaendelea kuliingizia taifa fedha za kigeni na kukuza uchumi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amesema kuwa Sekta hiyo inakuwa kwa kasi kubwa.

Amesema kuwa hali hiyo inatokana na kuongezeka kwa idadi kubwa ya watalii wanaokuja nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali ambapo mwaka jana waliingia watalii milioni 1.2.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati wa kukabidhi vyeti vya kutambua hadhi ya baadhi ya hoteli za kitalii  hapa nchini.

“Biashara ya hoteli inachangia pato la taifa kwa asilimia 25, hivyo ni muhimu katika kuongeza pato la taifa kwa kuvutia watalii wengi nchini,”amesema Prof. Maghembe.

Hata hivyo, kwa upande wake Mwenyekiti Shirikisho la vyama vya Utalii Tanzania (TCT), Abdulkadir Mohamed ameahidi kuendelea kuboresha huduma za hoteli hapa nchini ili ziweze kuendelea kuwa kivutio kikubwa kwa watalii.

?Live: Yanayojiri Moshi katika maadhimisho siku ya wafanyakazi Duniani
Magazeti ya Tanzania leo Mei 1, 2017