Waendesha mashtaka wa kesi ya Robert Sylevester Kelly (R. Kelly) wamesema kuwa mwanamziki huyo ametumia uongo, ujanja, vitisho na unyanyasaji wa kimwili kuwatawala waathiriwa hao na kuepuka uwajibikaji wa miaka.

Ushahidi huo umetolewa kwenye kesi inayomkabili R Kelly inayoendelea katika mahakama iliyopo  Brookyn, New York nchini Marekani. R. Kelly anatuhumiwa kwa ulaghai, unyanyasaji wa kijinsia na Rushwa mashtaka ambayo amekanusha mara kwa mara.

Baadhi ya madai yaliyotolewa dhidi ya mwimbaji huyo yaliyoanza Zaidi ya miaka 20,  Kelly anakabiliwa na mashtaka kwamba alikuwa kiongozi miongo miwili aliyetumika  kuajiri wanawake na wasichana wa umri mdogo kwa ajili ya ngono.

 Shahidi wa kwanza, Jerhonda Johnson Pace, aliwaambia majaji R. Kelly alimjua alikuwa na umri mdogo mwaka 2009 wakati walipofanya ngono huko Chicago, ambapo umri wa idhini ni miaka 17.

“Nilikuwa mwenye wasiwasi. Nilihisi kama haikuwa sawa, nikamwambia umri wangu.Aliniuliza , Hiyo inamaanisha nini? ” na akaniambia nimwambie kila mtu nilikuwa na miaka 19 – na niigize kuwa nina miaka 21,” Amesema Pace.

Katika hoja yake ya ufunguzi, wakili wa R. Kelly, Nicole Blank Becker amedai kuwa washtaki hao ni watu ambao awali walikubali kufanya ngono kabla ya baadaye kuwa wenye chuki.

R Kelly anaweza kuhukumiwa kifungo cha miongo kadhaa gerezani ikiwa atakutwa na hatia.

Kim Poulsen ataja kikosi Taifa Stars
Bangala kujiunga na wenzake leo usiku