Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa uvumi wa kuwa anaweza kuondolewa madarakani kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye utaharibu uchumi wa nchi hiyo.

Ameyasema hayo wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha Fox & Friends ambapo amesema kuwa masoko yataporomoka na kila mtu atakuwa maskini endapo watadiriki kumuondoa madarakani.

“Sijui ni kwa njia gani mtamtoa madarakani mtu ambaye amefanya kazi nzuri, ninawaambia hivi, kama nitaondolewa madarakani nadhani masoko yote yataporomoka kiuchumi, pia kila mtu atakuwa maskini,”amesema Trump

Aidha, Trump anakabiliwa na kashfa ya kumuamuru mwanasheria wake wa zamani, Michael Cohen kuwalipa fedha za uchaguzi wanawake wawili nyota wa filamu za ngono, Stormy Daniaels na Karen McDougal ambao wote walidai kuwa na mahusiano na Trump, hivyo ikalazimu awalipe fedha za uchaguzi ili wasiweze kumharibia katika kampeni za kuwania urais wa nchi hiyo.

Hata hivyo, mwezi Julai mwaka huu mwanasheria wa zamani wa rais huyo, Michael Cohen alitoa kanda ya sauti yake na Trump wakizungumzia moja ya malipo hayo kabla ya uchaguzi, huku mwanasheria huyo akiendelea na msimamo wake kuwa alifanya malipo hayo kwa wanawake wawili wakati wa kampeni ya urais ya mwaka 2016.

 

 

 

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 24, 2018
CCM Iringa: Mchungaji Msigwa ajiandae Kisaikolojia kuachia jimbo