Serikali ya Saudi Arabia inamchunguza mwanamitindo mmoja aliyejirekodi akiwa amevaa skerti fupi na tisheti kisha kuposti mtandaoni kitu ambacho ni kinyume na tamaduni ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Mwanamitindo huyo anayejulikana kwa jina la Khulood alisambaza video hiyo huku akitembea katika ngome ya kihistoria ya Ushayqir iliyopo nchini humo ambapo imelalamikiwa na baadhi ya wananchi wa nchi hiyo.

Aidha, Katika video hiyo iliosambazwa katika mtandao wa Snapchat wikendi iliopita, Khulood anaonekana akitembea katika barabara isiyokuwa na watu katika ngome hiyo ya historia ya Ushayqir iliyopo  kilomita 155 kaskazini mwa mji mkuu wa Riyadh mkoani Najd.

Hata hivyo, Video hiyo ilichukuliwa na watumiaji wa mtandao wa Twitter nchini humo ,ambapo kulikuwa na mjadala mkali kati ya wale wanaoamini Khulood anapaswa  kuadhibiwa na wengine walisisitiza kuwa aachwa huru avae anachotaka.

Jafo ang'aka, awataka maafisa elimu kuboresha mazingira ya shule nchini
Prof. Mbarawa: wananchi waliopisha ujenzi wa barabara watalipwa kwa mujibu wa sheria