IGP Sirro ameeleza hayo leo Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa takwimu za sasa zinaonyesha matukio ya aina hiyo yamekithiri sana nchini Tanzania jambo ambalo jamii inapaswa kubadilika ili kupunguza matukio hayo.

“Kuna makosa ambayo watu lazima wabadilike na hili haliitaji Jeshi la Polisi maana mimi nasimamia  Sheria lakini kuna viongozi wa dini wazungumzie hayo mambo. Muumini wako akija Kanisani au Msikiti na ukimwambia katazo la Mungu anaweza akabadilika”, alisema IGP Sirro.

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Sirro amesema kuna makosa ambayo viongozi wa dini wakishiriki kwa ukaribu zaidi inaweza kupunguza huku akiitaka jamii kubadilika kitabia ikiwemo kuachana na ulevi wa kupindukia.

Rihanna akataliwa kuingia Ghana, wadai ni ‘Freemason’
Serikali kutoa chanjo ya Saratani ya Shingo ya kizazi