Muigizaji wa filamu za Kiswahili, Steve Nyerere amedai kuwa kuna watu wasiojulikana wanamtafuta wakitaka kumdhuru.

Steve ametumia ukurasa wake wa Instagram kueleza jinsi anavyopata wakati mgumu hivi sasa kutokana na hatua za watu hao, huku akidai kuwa hajawahi kuogopa maisha yake kufikia kikomo.

“Maisha yangu yapo hatarini sijui kesho yangu, Ninapofika nyumbani kwangu naambiwa napewa na ujumbe kuna Watu wanakutafuta, nimekuwa kama yatima kwa Muda? Lakini niseme mimi ni mimi na mtabaki kuwa mimi sijawahi ogopa sijawahi tishika nilizaliwa siku 1 na mtakufa Siku moja ,Ndoto yangu ni kuwa , Ndoto yangu wanangu wasihishi kwa misaada wajue BABA yao ni zaidi ya BINADAMU ,Naipenda TANZANIA YANGU na hapa ni nyumbani kwangu Huzuni hujenga ujasili daima,” ameandika.

Hata hivyo, muigizaji huyo hakueleza kama ametoa taarifa juu ya watu hao kwenye vyombo vya dola au la.

Dar24 imejaribu kumtafuta mwigizaji huyo kwa njia ya simu lakini hadi habari hii inaandikwa, simu yake haikupatikana.

Hakuna kazi ngumu kama ya kuteua au kutengua- Ndugai
Uganda yampiga marufuku rafiki wa Bobi Wine kukanyaga ardhi yake

Comments

comments