Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassana amezindua Mpango Mkakati wa Water AID Tanzania ambao utasaidia upatikanaji wa maji safi na salama .

Uzinduzi huo umefanyika mapema hii leo jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge, Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo, Mkurugenzi wa Water Aid Kanda ya Afrika Mashariki. Olutayo Bankole –Bolawole, Mkurugenzi wa WaterAid Tanzania Dkt. Ibrahim Kabole na wadau mbali mbali wa maji, afya na mazingira.

Amesema kuwa Mpango wa Water Aid Tanzania wa miaka mitano utawezesha kuiweka Tanzania kwenye ramani ya matumizi endelevu ya rasilimali ya maji na utachangia katika utekelezaji wa malengo yaliyowekwa ya kupeleka huduma ya maji safi na salama kwa wananchi kulingana na Sera ya Maji.

Aidha, amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbali mbali imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika maeneo ya vijijini na mijini ambapo kwa mwezi Juni 2017 jumla ya watu 22,952,371 sawa na asilimia 72.58 ya wananchi waishio vijijini wanapata maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kama sera ya maji ya mwaka 2002 inavyoelekeza.

Hata hivyo, Makamu wa Rais amewaagiza wanaohusika na usimamizi wa miradi ya maji na usafi wa mazingira kuongeza jitihada zaidi ifikapo 2020 idadi ya wananchi wanaopata maji iwe imeongezeka kufikia malengo tuliyojiwekea.

 

Majaliwa aagiza Kapunga na wenzake 11 wakamatwe
Video: Mbowe anena mazito kuhusu uchumi, asema bandari ya Dar imekufa