Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetoa taarifa kwa Umma, Taasisi za Elimu ya Juu na Wadau wote wa Elimu kwamba maombi ya kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini kwa Shahada ya Kwanza yameanza rasmi julai 15, 2019 hadi Agosti 10, 2019.

Kwa hatua hiyo TCU imeamua kuviachia baadhi ya vyuo vikuu vilivyofungiwa udahili mwaka jana na awamu hii kuruhusiwa kufanya udahili mara baada ya kukidhi vigezo vilivyotakiwa.

Baadhi ya vyuo vilivyofunguliwa kuwa ni Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), Chuo kikuu kishiriki cha Marian cha Bagamoyo, Chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala (KIU) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mkuu Mihayo (AMUKTA). Huku akiahidi majina ya vyuo vingine vilivyoondolewa kwenye kifungo hicho kutajwa baadaye.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Uratibu na Udahili wa tume hiyo, Dk Kokuberwa Katunzi-Mollel ambaye amesema dirisha la udahili limefunguliwa kwa awamu ya kwanza na amewataka wanafunzi wanaotaka kujiunga na elimu ya juu kuanza dahili huo mapema kwani kazi kubwa ya TCU ni kusimamia uratibu.

Aidha, tume imeendelea kutoa elimu kwa umma kwa njia mbalimbali. Katika kipindi cha mwezi Juni na Julai, 2019 na imefanikiwa kutembelea Kambi zote za Jeshi la Kujenga Taifa na kutoa elimu kwa vijana waliohitimu kidato cha sita wanaoshiriki mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria. Aidha Tume kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali iliandaa na kuendesha programu maalum ya elimu kwa umma kuhusu taratibu za udahili mjini Unguja na Pemba.

 

Ashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kubaka na kulawiti
Dkt. Kolimba aendesha harambee kuchangia Ujenzi wa Kanisa Njombe