Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ( TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa katika Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka hiyo, mvua kubwa inatarajiwa kunyesha katika mikoa hiyo Januari 23 na 24 mwaka huu. Aidha, mvua itaendelea katika baadhi ya maeneo mikoani Lindi, Ruvuma na Mtwara Jumamosi tarehe 25 Januari 2020.

Mbali na mvua kubwa, TMA pia imetoa tahadhari ya upepo mkali na mawimbi katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, Dar es Salaam, Tanga, Unguja na Pemba.

Magufuli akaribisha Taasisi za nje kushuhudia uchaguzi mkuu Oktoba

Athari ambazo zinaweza kutokea ni pamoja na kuathirika kwa shughuli za uvuvi, changamoto ya usafiri na kuanguka kwa miti.

Mamlaka hiyo imetoa wito kwa Wananchi kuchukua hatua ili kuepuka athari ambazo zinaweza kujitokeza.

NEMC yanasa mifuko feki Njombe
Magufuli akaribisha Taasisi za nje kushuhudia uchaguzi mkuu Oktoba