Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa Iran itakuwa katika wakati mgumu iwapo itaanza kutengeneza silaha za nyuklia kufuatia Marekani kujitoa katika mkataba wa kimataifa wa 2015 uliokuwa unania ya kuizuia Tehran kuendeleza programu yake ya nyuklia.

Trump amesema kuwa Marekani itarejesha vikwazo vya uchumi katika juhudi za kuilazimisha Iran kufanya mazungumzo mapya juu ya mkataba huo, ikiwa ni pamoja na majaribio yake ya makombora ya ballistic na harakati zake za kijeshi huko Syria, Yemen na maeneo mengine Mashariki ya Kati.

Aidha, Kiongozi huyo wa Marekani ameituhumu Iran kuwa ndio chanzo cha migogoro katika ukanda wa mashariki ya kati kwa kufanya uchochezi baina ya nchi moja na nyingine.

“Sisi tutaingia katika mkataba mzuri sana au hatutakuwa na mkataba wowote ,” amesema. Trump amekiri kuwa Marekani huenda isifanye vizuri sana katika kufikia makubaliano.

Hata hivyo, maoni ya Trump yamekuja mara baada ya nchi tano zilizosaini mkataba huo, Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Russia na China zote zikisema kuwa zinaunga mkono mkataba huo.

 

 

Serikali yazindua chanjo ya kudhibiti Ukimwi kwa 90%
Sugu, Masonga waachiwa huru