Ni kama Cardi B na Nicki Minaj hawatamalizana leo au kesho kwani bado wanapashana joto la nani zaidi.

Siku chache baada ya kudaiwa kuwa Nicki alimtupia dongo rapa huyo wa kike kwenye ‘Ganja Burns’ ambayo iko ndani ya albam yake a ‘Queen’, Cardi anadaiwa kurejesha mbele ya kadamnasi.

Ni hivi, baada ya Cardi kukabidhiwa nafasi ya kwanza ya kufungua tuzo za MTV VMAs mwishoni mwa wiki, ilikuwa kama kichaa alipewa rungu kwa muda ambalo alilificha na kulitumia mwishoni.

Cardi ambaye alipanda na kitu ambacho alikifunga kama mtoto na baadaye kukifungua kwa mbwembwe na kubainika kuwa ilikuwa tuzo ya MTV, alinena mengi lakini mwisho alimpa ya uso Nicki Minaj.

Cardi alihakikisha amevuta usikivu wa watu wote, ofcourse akiwemo Nicki ambaye alikuwa amekaa kwa watazamaji, kisha akasema ‘I am the Empress’. Impress ni jina la mtawala wa kike wa ufalme/utawala fulani. Ana nguvu zaidi ya Malkia kwenye utawala wake.

Kauli hiyo ilionekana kama jibu kwa Nicki Minaj ambaye albam yake inambatiza jina la ‘Queen’ yaani Malkia. Na kwenye nyimbo nyingi anasikika akijigamba kwa wanamuziki wengine wa kike kuhusu hilo.

“Cardi amejiita ‘Empress’. Empress ana nguvu na ana watu wengi chini ya utawala wake zaidi ya Malkia. Sasa tumuite ‘Empress Cardi B’ kuanzia sasa,” alitweet shabiki mmoja.

Cardi aliyekuwa anaongoza akitajwa mara kumi kwenye orodha ya wanaowania, alishinda tuzo kadhaa ikiwa ni pamoja na msanii bora mpya, nyimbo bora ya ushirikiano na video bora ya msimu wa kiangazi.

Kwa upande wa Nicki, alibeba tuzo nzito ya wimbo bora wa Hip Hop kupitia ‘Chu Li’.

 

Wakili ajitoa kesi ya vigogo wa Chadema
Odinga kuwania tena urais 2022