Mbunge wa Nzega Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hussein Bashe amesema kuwa hawezi kumtupa wala kumsahau Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa kwa sababu amejifunza mengi kutoka kwake.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akifanya mahojiano na kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo cha Luninga cha Cloudstv.

Bashe amesema kuwa kazi kubwa ya bunge ni kuisimamia serikali ili iweze kutoa huduma stahiki kwa wananchi, hivyo ni jukumu la kila mbunge kutimiza wajibu wake akiwa ndani ama nje ya bunge.

Hata hivyo, Bashe ameongeza kuwa huwa anasimamia kile ambacho anakiamini pia huikosoa na kuilinda serikali ya yake ya chama cha mapinduzi. CCM

Video: Tanzania ni kitovu cha ukombozi wa Bara la Afrika- Dkt. Mwakyembe
ACT yatao pongezi kwa baraza la maaskofu

Comments

comments